KUANZA NA UKUAJI WA BRAND
ASILI YA BRAND
Usiku mmoja, nilikuwa naongea na mtu kuhusu maswala nayofanya na badala yake akanifungua macho juu ya kitu kinaitwa "Branding" na mwengine alinishauri zaidi juu ya "Online Presence"
Tangia siku hiyo, maono yangu juu ya ndoto nilizonazo hazikubadilika, badala yake ziliboreshwa.
Branding ni kitendo cha mtu binafsi kujitangaza kama chapa, wakiangazia sifa zao za kipekee ili kujitokeza katika nyanga zao. Kwa kuzingatia hivyo nikaamua kutengeneza logo yangu ambayo imekaa kipekee. Brand inaitwa MUHAMAD KASSIM: GAME OPTIMIZING AND MAINTENANCE japo huduma zilizopo ni zaidi ya hayo. Kwa kuona kuwa naweza jitangaza na kujulikana na watu kulingana na kile nachoweza fanya, sikufikiria mara mbili zaidi ya kuchukua fursa.
Baadhi ya watu hushindwa kuelewa inachukua muda mrefu sana mpaka brand yako kujulikana au hata mtu binafsi kujulikana kulingana na unachofanya ima bado unasoma ama upo tu mtaani. Namna utakavyoishi na watu, mada utakazozungumza na hata vitu utakavyosaidia vitawawapa majibu juu ya kile ulichobobea.......pengine wakaona hata vitu ambavyo hujawahi dhania ulivyo navyo.
Isingekuwa kwa wahusika tofauti kuchangia juu ya kile nachofanya(majina yao nitayahifadhi mpaka pale watakapotaka kujulikana) basi hii ndoto ingeishia kwenye makaratasi na mdomoni japo bado ina safari ndefu sana katika ukuaji.
⚙️MUHAMAD KASSIM: GAME OPTIMIZING AND MAINTENANCE
Hii sio kampuni hivyo basi ni brand ya mtu binafsi, nina endesha kila kitu peke yangu. Jina la brand linatokana na jina langu binafsi(Muhamad Kassim) na huduma kuu mbili zinazopatikana(Game Optimization and Maintenance). Nitaelezea huduma zote ambazo nazotoa kulingana na ujuzi wangu wa IT.
@. Game Optimization(Uboreshaji wa Mchezo): Huu ni mchakato wa kubadilisha mipangilio ya programu na vifaa ili kuongeza utendaji wa mchezo uliokwisha tengenezwa (ready-made game) bila kuhariri msimbo wa msingi wa mchezo. Lengo kuu ni kuhakikisha mchezo unachezwa kwa kasi, uthabiti, na ubora wa picha unaolingana na uwezo wa kifaa cha mtumiaji. Anayefanya mchakato huu anaitwa "GAME OPTIMIZER".
Anaweza kuja mtu na laptop, PC au simu yake. Ninaangalia uwezo wake katika kila kipengele na baada ya hapo naangalia ni magemu gani ambayo anaweza cheza kwa ufanisi mzuri zaidi baada ya kukwisha ziseti.
Mfano,mimi natumia laptop aina ya HP PROBOOK 440 G5, ina CPU generation ya 8 lakini ina RAM ambayo ni single channel(Speed yake inafika ~19GB/s) ila magemu ambayo ninayacheza unahitaji PS4(RAM ya PS4 ya kawaida ni 8GB ila inafika speed zaidi ya 75GB/s!). Zipo games kama Resident Evil 6, Metal Gear Solid V: Ground Zeroes(Gameplay yake ipo YouTube), Dirt Rally, Grand Theft Auto V, Need For Speed Payback, Battlefield 4, Call of Duty: Ghost na Mad Max, kwa uchache sana!!!
Alishawahi kuja mtu na laptop yenye muundo wa tablet alafu inatumia passive cooling(hizi laptop hazina feni). Iliweza kucheza Battlefield 4 na Dirt Rally(video zipo tiktok, ni za mwanzo kabisa kupostiwa) na ilizicheza hali ya kuwa inatumia betri yake na sio kwenye umeme. Kumbuka haya ni magemu mazito sana ndio maana zipo toleo la PS4
@. Maintenance(Matengenezo): Kama ambavyo jina linavyosema, huu ni mchakato wa kuhifadhi, kurekebisha, au kuboresha vifaa, programu, au mifumo ili viendelee kufanya kazi vizuri na kwa usalama. Matengenezo yanaweza kuwa ya mara kwa mara (preventive), ya kurekebisha (corrective), au ya kuboresha (upgrading).
Michakato hii unaweza fanya upande wa hardware kama kutengeneza ama kubadilisha vifaa vya umeme vya kompyuta au simu na upande wa software kama kuangalia app gani unayohitaji kwa ajili ya kufanya kazi husika kulingana na kifaa chako. Game Optimization inatumia ujuzi wa Maintenance japo yenyewe kuifahamu kuna vitu lazima uvijue kiundani. Maintenance ni moja kati ya sababu kwanini inakuwa ni rahisi kuwa fundi umeme kwa kiasi fulani au pengine kuzama kabisa katika kipengele hicho.
Kwa mimi, ninafanya software na hardware maintenance kwa kompyuta na software maintenance kwa simu.
@. IT Consultation(Ushauri wa IT):Ushauri wa TI (Technology Integration Consultation) ni huduma ya kitaalamu inayolenga kusaidia watu binafsi, mashirika, au taasisi kuunganisha teknolojia mpya au zilizopo katika mazingira yao ya kazi, elimu, au biashara kwa njia bora na yenye tija.
Kwa kuwa ni mbobezi na mtaalam wa IT kulingana na huduma nazotoa, natoa pia ushauri na mbinu za kufahamu namna gani ya kutumia aina fulani ya teknolojia na jinsi gani inaweza kuwa na manufaa kwako.
UPATIKANAJI
Unaweza kunipata kwenye link-in-bio yangu, ambayo ina link za mitandao mengine yote(WhatsApp, Instagram, Tiktok, YouTube na Facebook)
Kuna tovuti ambayo imeshika hizi zote pamoja na contact za WhatsApp, ila pia hiyo tovuti ni kwa ajili ya watu watakaohitaji games ili waweze kuona magemu yaliyopo pamoja na bei zake.


Comments
Post a Comment